Galana primary school ni shule iliyofika darasa la tano kwa sasa na iko na shule ya chekechea. Jambo la kushangaza ni kwamba tumeingia katika darasa moja linalosoma darasa la nne na la tano,yaani walimu wawili wa masomo tofauti wanafunza darasa moja.Huku watoto wa chekechea wakihifadhiwa kwenye kanisa lenye paa peke yake bila kuzibwa ukuta na halina simiti wala viti jambo ambalo huenda likasababisha mkurupuko wa maradhi na hata pia funza.Ijapokuwa CDF na LATF zimejenga madarasa mawili kila moja,lakini kuna haja ya madarasa mengine kuongezwa na viti ili kuwafanya wanafunzi hao kusoma katika mazingira yanayostahili.

Advertisements